Mohamed Maatouk

WAJERUMANI KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA MBOLEA MTWARA

WAJERUMANI KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA MBOLEA MJINI MTWARA

Mohamed Maatouk
Mwakilishi wa kampuni ya HELM A.G  katika bara la Africa Mohamed Maatouk.

Kampuni ya HELM A.G ya nchini Ujerumani imeanza maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea, kitakachojengwa katika kijiji cha Msanga Mkuu wilaya na mkoa wa Mtwara na kugarimu dola za kimarekani bilioni mbili kitakapokamilika.

Mwakilishi wa kampuni ya HELM anayeshughulika na miradi ya uzalishaji bidhaa zinazotokana na taka petrol katika bara la Afrika Mohamed Maatouk, alitoa taarifa hiyo kwenye kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Mtwara na viongozi wengine wa serikali,kilichofanyika katika ukumbi wa boma mjini humo hivi karibuni.

Alisema kiwanda hicho ambacho kitajengwa kwa awamu nne,ujenzi wa awamu ya kwanza unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu na kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kwa mujibu wa bw. Maatouk ujenzi wa awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ukikamilika kitatengeneza nafasi 600 za ajira za moja kwa moja,tofauti na miradi mingine mradi huo utamilikiwa kwa ubia kati ya kampuni yake na halmashauri za wilaya katika mkoa huo.

Kulingana na mwakilishi huyo wa kampuni ya HELM amani na utulivu wa kiasiasa wa nchi ya Tanzania na kuwepo mazingira mazuri ya uwekezaji katika mkoa wa Mtwara ikiwemo mali ghafi,ni kivutio kilichosukuma kampuni yake kufikiri na kufanya uamuzi kuwekeza hapa nchini.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa katika kipindi cha miaka kumi hadi kumi na mitano kiwanda kitakachojengwa kitaendeshwa kwa asilimia mia moja na wataalam na nguvu kazi ya Tanzania” alisisitiza Maatouk.

Akizungumza katika kikao hicho aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa Mamlaka Ya unendelezaji Maeneo huru ya Uzalishaji bidhaa za kuuza nje ya nchi EPZ ,knl mstaafu Joseph Simbakalia, alisema mkoa wa Mtwara unayo nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji wengi kutokana na ukweli kwamba mkoa huo ni pekee hapa nchini,mwekezaji akihitaji eneo la kuwekeza linapatikana na hakuna fidia kwani mamlaka ya bandari nchini ina eneo kubwa ambalo ilitoa fidia kwa wamiliki wa zamani wa eneo hilo.

“Mkoa wa Mtwara ni mkoa pekee akija mwekezaji na kusema mimi nahitaji ekari mia moja za kiwanda,nazungumzia EPZA sasa;baada ya kupewa eneo hilo,nitamwambia twende,hakuna fidia maana bandari walikwishatoa fidia.Eneo liko wazi,kwingine kote wanakwenda wanaanza kuzungumza,tuelewanae na wananchi miezi sita mwaka;wengine hawana subira,anasema bwana mimi nawapeni miezi miwili kama hamuwezi basi ntakenda Kenya,ntakwenda wapi wengine hawana subira”Alisisitiza Simbakalia.

Mkurugenzi wa EPZA alikwenda mbali na kubainisha kwamba huhitaji kuwa mtabiri kujua kwamba kama hali ya amani itaendelea jinsi ilivyo sasa hapa Tanzania,na hali ya Mtwara,katika nchi za Afrika mashariki na kati mji mkubwa wa viwanda katika ukanda huu utakuwa ni mji wa Mtwara.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi mheshimiwa Hawa Ghasia na mkuu wa mkoa huo mh.Halima Debdegu waliwataka wananchi wa mkoa huo kuwa watulivu na kuhakikisha amani inakuwa endelevu ili kuendelea kuvutia fursa zaidi za wawekezaji kutoka nje ya nchi.Kwa nyakati tofauti walisisitiza kuwa hatua hiyo ya kuwepo kwa amani na utulivu itasaidia sana kuongeza nafasi za ajiria na kupunguza umaskini katika jamii.

Aidha mkuu wa mkoa wa Mtwara aliwataka wananchi hasa vijana kuwa watulivu na kuhakikisha wanajielimisha katika maswala mbalimbali kupitia elimu rasmi na elimu ya maisha, ili waweze kuendana na mabadiliko yatakayoletwa na uwekezaji huo na ule unaokuta.

Kiwanda hicho cha mbolea kitakuwa ni uwekezaji wa pili mkubwa tangu gesi kugunduliwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi,kikitanguliwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha saruji cha mwekezaji kutoka nchini Nigeria Aliko Dangote ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake miezi michache ijayo, ujenzi unaoendelea utakapokamilika.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi mh. Hawa Ghasia,mkurugenzi wa EPZ knl mstaafu Joseph Simbakalia,Mkuu wa mkoa wa Mtwara bi Halima Dendegu  na viongozi wengine wa mkoa wa Mtwara na serikali wakisoma ramani na kusikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya HELM A G ya Ujerumani bw. Mohamed Maatok katika kijiji cha Msangamkuu wilayani Mtwara
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi mh. Hawa Ghasia,mkurugenzi wa EPZ knl mstaafu Joseph Simbakalia,Mkuu wa mkoa wa Mtwara bi Halima Dendegu na viongozi wengine wa mkoa wa Mtwara na serikali wakisoma ramani na kusikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya HELM A G ya Ujerumani bw. Mohamed Maatok katika kijiji cha Msangamkuu wilayani Mtwara

Philipo Lulale          email:maishanifursa@gmail.com        +255762128899

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s